Wachunguzi wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) wamegundua mwili wa mwanamke ukiwa umeoza katika nyumba moja iliyoko eneo la YMCA huko jijini Nakuru.Uchunguzi wa kina uliofanywa na polisi umebaini kwamba kifua cha mwanamke huyo kilikuwa kimefungwa kwa nakala ya Biblia. Nyumba hiyo, ambayo ni mali ya Bw. David Kinyanjui na mkewe mpya, imegeuka kuwa eneo la uhalifu ambalo polisi wanachunguza kwa makini. Tukio hili limezua maswali mengi….CONTINUE READING
Hali hii ilianza wakati Rosemary Wahu, dadake Bw. Kinyanjui mwenye umri wa miaka 60, alipowatembelea wanandoa hao huko Nakuru. Kulingana na mwana wao, Bw. Boniface Mwangi, mamake alifanya ziara hiyo mnamo Januari 15, 2024, baada ya kuarifiwa kuwa Bw. Kinyanjui alikuwa ameoa tena miezi michache baada ya kutengana na mke wake wa awali.
Bw. Kinyanjui alitaka wawili hao wakutane. Bi. Wahu aliondoka nyumbani kwake Kaunti ya Kiambu na kuelekea Nakuru kumtembelea nduguye. Aliiambia familia yake kwamba alikuwa amewasili salama.
Hata hivyo, mawasiliano kati ya Bw. Mungai na mamake yalikatika ghafla mnamo Januari 29, 2024. Bw. Mungai alipojaribu kumpigia simu mjombake kuuliza kuhusu mamake, Bw. Kinyanjui alianza kutoa maelezo yasiyoeleweka, akisema simu yake ilikuwa imeanguka majini na kuharibika.
Baada ya siku kadhaa za mvutano, Bw. Mungai alisisitiza kuzungumza na mamake, ingawa Bw. Kinyanjui alikataa. Hali hii ilizua maswali zaidi.
Jumanne, jirani mmoja wa Bw. Kinyanjui alimwambia Bw. Mungai kuhusu harufu mbaya iliyokuwa ikitoka nyumbani kwake. Pia, alimjulisha kwamba Bi. Wahu hakuonekana kwa zaidi ya wiki mbili, jambo lililowatia wasiwasi jamaa zake.
Bw. Mungai na familia yake waliamua kusafiri hadi Nakuru kuchunguza kile kilichokuwa kikijiri. Walipofika nyumbani kwa Bw. Kinyanjui, waligundua mwili wa Bi. Wahu ukiwa umeoza na nakala ya Biblia iliyofungwa kwenye kifua chake.
“Inaonekana kuna uwezekano alifariki wiki mbili zilizopita. Kuna harufu mbaya kote katika chumba hicho. Tunawaomba polisi kufanya uchunguzi wa haraka ili kubaini chanzo cha kifo hiki tatanishi,” alisema Bw. Zack Wanjohi, jamaa wa marehemu.
Bi. Penninah Wambui, jirani, alisema kuwa Bw. Kinyanjui na mkewe walidai harufu hiyo ilitokana na mzoga wa mbwa aliyekufa na kwamba walikuwa wakisubiri ufufuo. Hata hivyo, jirani hawakuelewa jambo hilo na waliona kuwa ni shughuli za kushangaza.
Mohamed Wako, Mkuu wa Polisi katika eneo la Nakuru Mashariki, alithibitisha kisa hicho na kueleza kuwa wameanzisha uchunguzi kubaini sababu ya kifo cha Bi. Wahu. Bw. Mungai na mkewe wamekamatwa kusaidia polisi katika uchunguzi wao.