‎MAAJABU!! Mwanaume amepatikana Akiishi na Ndoo za Kinyesi na Lita 40 za Mkojo Ndani ya Single Room -
Bizzare

‎MAAJABU!! Mwanaume amepatikana Akiishi na Ndoo za Kinyesi na Lita 40 za Mkojo Ndani ya Single Room

.

‎Wakazi wa mtaa mmoja walipigwa na butwaa baada ya mwanaume kupatikana akiishi kwenye nyumba ya single room iliyokuwa imejaa uchafu wa kutisha. Ndani ya nyumba hiyo, kulipatikana ndoo kadhaa zikiwa zimejaa kinyesi na zaidi ya lita 40 za mkojo zilizohifadhiwa kwenye chupa ndogo ndogo.

‎Majirani walisema walikuwa wakihisi harufu mbaya kwa muda mrefu lakini wakashangaa kwa nini jamaa huyo hakuonekana akiingia choo cha ploti. Walipoamua kumlazimisha afungue mlango, walikumbana na hali ya kusikitisha ambapo kinyesi kilikuwa kimetapakaa sakafuni huku chumba hicho ndicho pia anapotumia kupikia na kulala.

‎Baada ya kuhojiwa, mwanaume huyo alikiri kuwa kwa zaidi ya miezi sita hajawahi kutumia choo cha kawaida na badala yake ukihifadhi kinyesi na mkojo ndani ya nyumba yake. Aliongeza kuwa amezoea mazingira hayo na hata hahisi harufu.

‎Cha kushangaza zaidi, jamaa huyo ni supervisor katika kampuni moja maarufu ya kutengeneza pombe, na kwa muonekano wake huwezi kudhani anaishi kwa uchafu wa kiwango hicho.