Anasema alikutana na msichana ambaye alimwambia anasoma Asumbi Girls. Kwa sababu ya umbo lake kubwa, alidhani ni mwalimu mtarajiwa aliyekuwa akifanya teaching practice. Kwa sura na umbo, alimkadiria kuwa na umri wa takribani miaka 25. Hata hivyo, baadaye ilibainika kuwa msichana huyo alikuwa na umri wa miaka 16 pekee.
Kosa hilo lilimpeleka mahakamani na hatimaye kuishia kifungoni kwa miaka 15. Akiwa gerezani, anawaonya wanaume wawe makini zaidi na vijana wa kike, kwa sababu umbo au mwonekano sio kipimo cha umri.
Amewashauri wanaume kuhakikisha wanathibitisha umri wa msichana kabla ya kuingia katika uhusiano wowote wa kimapenzi, akisisitiza umuhimu wa kuomba kitambulisho cha taifa au cheti cha kuzaliwa.
Kisa hiki kinatilia mkazo ukali wa sheria za Kenya kuhusu defilement, na kwamba kutojua umri wa mhusika sio kinga mbele ya sheria. Ni somo la tahadhari kwa jamii nzima kuhusu umuhimu wa tahadhari, uwajibikaji na kuheshimu mipaka ya kisheria.