gossips

Hakuna kitu kigumu kama kulea mtoto anayefanana na baba aliyemkataa – Carrol Sonie

Muigizaji Carrol Sonie amefunguka jinsi ambavyo amekuwa akiumia ndani kwa ndani kumlea bintiye Keila ambaye anafanana na baba ambaye alimkataa – Mulamwah.

Sonie kupitia kipindi cha maswali na majibu na mashabiki wake kwenye chaneli ya YouTube, mmoja alimuuliza changamoto kuu ambayo amekuwa akipitia katika malezi ya bintiye.

Sonie alisisitiza kwamba hajawahi shirikiana katika malezo na mtu yeyote [Mulamwah] akisema kwamba watu pekee ambao wanamsaidia katika kumlea Keila ni wazazi wake tu.

Alisema kwamba kama kuna kitu kinachomkereketa moyo wake kila anapomtazama malaika wake usoni ni kugundua kwamba anamfanana Mulamwah hali ya kuwa alimkataa kuwa si mwanawe.

“Sijui kama inauma ama nini, lakini mashabiki wangu, haswa kina mama, hebu tafakari kulea mtoto wako ambaye amekataliwa halafu sura yake ni ya babake? Unafanya nini katika hali kama hiyo? Unajipa moyo na kusonga mbele haijalishi,” Sonie alisema.

Sonie pia alithibitisha kwamba ana mpenzi na amesonga mbele na maisha yake kutoka kwa kile kilichojiri mitandaoni kwa miezi kadhaa baada ya kuachana na Mulamwah.

Alisema kwamba siku atakuja kuamua kumtambulisha mpenzi wake, dunia nzima itasimama, lakini pia akaweka wazi kwamba hana lolote la kufanya na Mulamwah kwani alishamkataa binti yake.

Sonie alisema alishaliondoa jina la Mulamwah kwenye cheti cha kuzaliwa, na aliyataja majina yote mapya kuthibitisha kwamba Mulamwah hana hata chembe katika maisha ya binti yake.

“Majina ya binti yangu yote si ya Kinngereza, anaitwaKeila Khoe Wangui Muthoni, ahsante sana kwa swali hilo,” Sonie alisema.